Mbosso Avunja Ukimya Vita Yake na Aslay!

Hivi karibuni kumekuwa na maneno ya chini kwa chini yakiwahusisha ugomvi uliokuwepo kati ya Mbosso na Aslay ambapo walikuwa ni wasanii wa zamani kutoka katika kundi moja la Yamoto Band.

Katika mahojiano aliyoyafanya Mbosso akiwa na IJUMAA WEEKEND, alifunguka kuwa hana ugomvi wala kinyongo chochote na Aslay, na pia haelewi ni nini kinachoendelea.

MIMI NA WENZANGU TULIOKUWA WOTE YAMOTO BAND, TUKO SAWA JAPOKUWA MAWASILIANO YETU NI HAFI FU NA KILA MMOJA ANA UONGOZI WAKE

MIMI SINA TATIZO, WATU WANATAKIWA WAJUE SINA TATIZO NA MTU, SIJUI NA WALA SIWEZI KUKAA NA KINYONGO NDANI, MAANA MIMI NI MWEPESI WA KUMWAMBIA MTU NENO SAMAHANI KULIKO NENO NAKUPENDA.

Baada ya mahojiano hayo alitafutwa Aslay ili kusikia kwa upande wake, lakini juhudi ziligonga mwamba na tulipomtafuta meneja wake Shaban Chambuso alisema kuwa Aslay yupo Zanzibar na pindi akirejea atawatafuta waandishi.

Chicco

Professional blogger, Wordpress designer, Developer and Innovator on digital ideas around the world. Vision of geoneb.com is to connect Music & Movie industry and fans in the same room easily.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button