Entertainment

Dudubaya Kizimbani kwa Kumchafua Kusaga

MSANII  wa Bongo fleva, Godfrey Tumaini (41) maarufu kama ‘Dudu Baya’, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shtaka la kutumia lugha chafu mtandaoni.

Wakili wa Serikali, Hilda Katto, amedai kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 11, 2020, ambapo aliandika lugha ya matusi kwa Joseph Kusaga katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kuisambaza.

Inaelezwa barua hiyo ilidai Joseph ndiye mmiliki wa Kituo cha Utangazaji cha Wasafi na amekisajili kwa jina la mke wake na anatumikishwa kuzalisha mashoga Tanzania.

Mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na upande wa Jamhuri umesema upelelezi umekamilika. Dudu Baya yuko nje kwa dhamana hadi Januari 28, kesi itakapotajwa tena.

Leave a Comment