BASATA yamtaka Diamond kuwatumia wasanii waliosajiliwa kwenye tamasha lake

Baraza la Sanaa Tanzania ( BASATA ) limewataka wasanii wote ambao watatumbuiza katika Tamasha la ‘Tumewasha’ linaloendeshwa na Wasafi Media kuhakikisha wamesajiliwa na baraza hilo ili kuwa na uhalali wa kupanda jukwaani.


Akizungumza na waandishi wa habari hii leo, Mkurugenzi Mtendaji wa ‘Wasafi Media’ Naseeb Nyange ‘Diamond Platnumz’ amesema wako tayari kufuata agizo hilo ili kuepuka kufungiwa kwa tamasha hilo litakalohusisha wasanii wa ndani na nje ya nchi.

“Tunatamani kuwa na wasanii wote, hivyo kwa wasanii ambao hawajasajiliwa na Basata wasajiliwe ili tuwe nao” amesema Diamond Platnumz.

Kuelekea tamasha hilo litakalofanyika Januari 30, 2020 Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam ‘Diamond’ amesema kuwa wasanii ambao hawajasajiliwa na wako tayari kufanya hivyo atawasaidia kujisajili kupitia tamasha hilo kw angalizo ‘Tumewasha Tour’

Chicco

Professional blogger, Wordpress designer, Developer and Innovator on digital ideas around the world. Vision of geoneb.com is to connect Music & Movie industry and fans in the same room easily.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button